IQNA

Harakati za Qur'ani

Shakhsia wa Mwaka wa Qur’ani Tukufu atajwa

19:27 - February 25, 2024
Habari ID: 3478413
IQNA - Astan (Mfawidhi) wa Haram tukufu ya Imam Hussein (AS) huko Karbala, Iraq, ilimtaja mwandishi mashuhuri wa kaligrafia, Uthman Taha kama shakhsia wa Qur'ani wa mwaka.

Sheikh Hassan al-Mansouri, mshauri wa Katibu Mkuu wa Haram tukufu ya Imam Hussein (AS), alisema uteuzi wa shakhsia wa mwaka wa Qur'ani ulifanywa kwa mwaka wa tatu mfululizo kwa lengo la kuwaenzi wale wanaotumikia Kitabu Kitukufu.

Alisema Dk Uthman Taha ni mwandishi mashuhuri wa maandishi ya Qur'ani, ambaye  mamilioni ya nakala za Mus’haf wake zimechapishwa na kusambazwa miongoni mwa Waislamu duniani kote.

Ameongeza kuwa katika kikao na Uthman Taha katika mji mtakatifu wa Madina, alifahamishwa kuchaguliwa kuwa shakhsia wa Qur'ani wa mwaka huo na kupewa cheti cha heshima.

Kulingana na al-Mansouri, Taha aliwashukuru maafisa wa Haram tukufu ya Imam Hussein (AS)  na kusema yuko tayari kuzuru Iraq ikiwa hali yake ya afya itaimarika.

Taha pia aliangazia ushawishi wa mwandishi wa kale wa Iraq Hashim al-Baghdadi katika maandishi ya Qur'ani.

Mwaka jana, Dk Fadhil al-Samiraei, mtafiti mashuhuri wa Qur'ani, alitajwa kuwa mtu bora wa mwaka wa Qur'ani.

Uthman ibn Abduh bin Husayn ibn Taha al-Halyabi (Uthman Taha) ni mwandishi wa Qur'ani wa Syria-Saudia katika lugha ya Kiarabu maarufu kwa kuandika kwa mkono Mus'haf al-Medina.

Alizaliwa mwaka wa 1934 katika eneo la mashambani la Mkoa wa Halab au Aleppo, Syria.

 

 

Quranic Personality of Year Named

Quranic Personality of Year Named

Quranic Personality of Year Named

 

 

3487326

captcha