IQNA

UNICEF

Boko Haram limeathiri maisha ya watoto milioni 1.4

17:08 - September 19, 2015
Habari ID: 3365086
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa idadi ya watoto waliolazimika kuyahama makaazi yao kutokana na mashambulio ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram ndani ya Nigeria na katika nchi jirani imefikia milioni moja na laki nne

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na shirika hilo la Umoja wa Mataifa, watoto wapatao laki tano walipoteza makaazi yao katika kipindi cha miezi mitano iliyopita baada ya kuongezeka ghafla mashambulio ya kundi hilo la kigaidi. Boko Haram, ambalo ni kundi lenye ufahamu potofu juu ya Uislamu, linaendesha uasi kwa mwaka wa sita sasa kwa lengo la eti kuunda dola la Kiislamu katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria. Hujuma na mashambulio ya kundi hilo la kigaidi na kitakfiri hadi sasa yamesababisha vifo vya maelfu ya raia na wengine milioni mbili na laki moja kubaki bila makaazi, akthari yao wakiwa ni watoto. Kwa mujibu wa taarifa ya UNICEF, katika eneo la kaskazini mwa Nigeria pekee, karibu watoto milioni moja na laki mbili, zaidi ya nusu yao wakiwa na umri chini ya miaka mitano, wamelazimika kuyahama makaazi yao. Watoto wengine 265,000 ni raia wa nchi jirani za Cameroon, Chad na Niger.

Neno Boko Haram kwa ya lugha ya Kihausa lina maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Kundi hilo la Boko Haram ambalo lina ufahamu usio sahihi na potovu kuhusu dini ya Kiislamu, limekuwa likitekeleza hujuma katika maeneo mbalimbali ya Nigeria hasa kaskazini mwa nchi hiyo.../mh

3364918

Kishikizo: watoto nigeria BOKO HARAM
captcha