IQNA

Turathi ya Kiislamu

Nakala Adimu ya Qur'ani ya dhahabu imezawadiwa Jumba la Makumbusho la Karbala (+Video)

21:27 - May 21, 2023
Habari ID: 3477028
TEHRAN (IQNA) – Jumba la Makumbusho la Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS huko Karbala, Iraq imekabidhiwa nakala adimu ya Qur’ani Tukufu iliyopambwa kwa dhahabu na fedha.

Mfuasi wa Ahl al-Bayt AS ambaye jina lake halikutajwa aliwasilisha nakala adimu ya Msahafu huo kwenye jumba hilo la makumbusho. Imepambwa kwa dhahabu, shaba, almasi, platinamu na fedha, shirika la habari la Iraq la Noon liliripoti.

Ghassan Shahristani, Jumba la Makumbusho la Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS, anasema kazi hiyo ya thamani imepakwa dhahabu ya karati 18 na 24. Pia ina gramu 1,500 za fedha safi, karatasi 21 za shaba na sahani za fedha na platinamu, na almasi ya karati 1.5, aliongeza.

Kiasi cha dhahabu kilichotumika kuunda katika Msahafu huo adimu  ni kilo nne na umeandikwa katika mwandiko wa Usman Taha.

Hii hapa chini ni klipu ya video Msahafu huo.

4141958

captcha