Abubakar Shekau kiongozi wa kundi la Boko Haram amesema katika mkanda wa video wa dakika 52 kuwa, ameasisi utawala wa Kikhalifa katika mji wa Gwoza baada ya kuuteka mapema mwezi huu.
Shekau ameongeza kuwa yeye na wanamgambo wa kundi la Boko Haram wamekuja kuishi katika mji huo na kwamba hawakusudii kuondoka katika mji huo.
Hata hivyo jeshi la Nigeria kwa upande wake limepingag madai ya kiongozi huyo wa Boko Haram juu ya kuuteka mji wa Gwoza.
Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo.
1443021