IQNA

Waislamu Ulaya

Msikiti Ugiriki wafunguliwa kwa Sala ya Idul Fitr baada ya karne

11:40 - April 12, 2024
Habari ID: 3478674
IQNA - Sala ya Idul Fitr iliswaliwa na zaidi ya waumini 100 wa Kiislamu katika Msikiti wa Yeni huko Thessaloniki, kaskazini mwa Ugiriki, siku ya Jumatano.

Ilikuwa ni mara ya kwanza msikiti huo kufunguliwa kwa ibada katika kipindi cha karne moja.

Msikiti wa Yeni uligeuzwa kuwa jumba la makumbusho mnamo 1925 kufuatia mabadilishano ya watu kati ya Ugiriki na Uturuki.

Siku ya Jumatano msikiti huo Wizara ya Utamaduni Ugiriki iliukabidhi msikiti huo kwa masaa machache kwa Wizara ya Elimu na Masuala ya Kidini kwa ajili ya Sala ya Idul Fitr.

Ulinzi ulikuwa mkali katika eneo hilo, ambalo lilikaribisha zaidi ya Waislamu 100 kuadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Msikiti mwingine wa kihistoria, wa Suleymaniye huko Rhodes, pia ulifunguliwa kwa ajili ya maombi siku ya Jumatano, huku Waislamu katika mji mkuu wa Ugiriki wakimiminika kwenye Msikiti mpya wa Athens katika wilaya ya kati ya Votanikos.

Kishikizo: msikiti ugiriki waislamu
captcha