IQNA

Muharram 1445

Waislamu wa Madhehebu ya Shia katika maombolezo ya Muharram mitaa ya New York (+Video)

18:46 - July 25, 2023
Habari ID: 3477338
TEHRAN (IQNA) – Maelfu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia waliingia kwenye mitaa ya New York katika maombolezo ya Muharram.

Watu kutoka mataifa mbalimbali kama vile Afghanistan, Iran, Tanzania na Pakistan walishiriki katika hafla hiyo iliyofanyika katika eneo la Manhattan  jijini New York siku ya Jumapili, IRIB iliripoti.

Tukio hilo hufanyika kila mwaka chini ya jina la Siku ya Hussein katika mwezi wa Muharram.

Inakadirwa kuwa Waislamu milioni mbili wa madhehebu ya wanaishi katika majimbo tofauti ya Marekani na wanafanya matukio kama hayo katika miji mbalimbali kila mwaka.

Mwezi wa Muharram, ambao ulianza Jumatano iliyopita, ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwandamo ya Hijria Qamaria.

Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengine katika sehemu mbali mbali za dunia hufanya sherehe kila mwaka katika mwezi wa Muharram kuomboleza kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na masahaba zake.

Imam Husain AS aliuawa shahidi kikatili na kinyama mwaka wa 61 Hijria Qamaria, , katika jangwa la Karbala, Iraq ya leo, akiwa na umri wa miaka 57 baada ya kuongoza mapambano ya kishujaa ya ushindi wa damu mbele ya upanga.

Vita vya Karbala vilikuwa moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq. Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi la batili ili kuilinda dini ya Allah. Hamasa ya Karbala ilikuwa dhihirisho la mambo mawili makuu.

Kwanza ni ujasiri, ushujaa, moyo wa kujitolea, uaminifu pamoja na kuyapokea kwa moyo mkunjufu mauti ya kuuawa shahidi, sifa walizojipamba nazo wapiganaji wachache wa jeshi la haki wakiongozwa na Imam Hussein AS dhidi ya Yazid bin Muawiya.

Pili ni upeo wa ukatili, udhalimu na unyama ulioonyeshwa na jeshi batili la Yazid bin Muawiya. Baada ya kupambana kishujaa, hatimaye mjukuu huyo wa Mtume Muhammad SAW aliuawa shahidi tarehe 10 Muharram katika siku ya Ashura.

3484485

captcha