IQNA

Jinai za Israel

Kampeni ya kura ya 'Sitisha vita Gaza' katika uchaguzi wa Marekani

15:26 - January 23, 2024
Habari ID: 3478238
IQNA - Wapiga kura wa Marekani wamehimizwa kuandika "Sitisha Vita Gaza" kwenye kura zao wakati wa kuchagua wagombea wa uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba ikiwa ni njia ya kubainisha malalamiko kuhusu jinsi Joe Biden alivyoshughulikia vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Gaza.

Harakati ya Kura ya 'Sitisha vita Gaza' ambayo ni  muungano wa vikundi vya kupinga inasema juhudi hizo zinawaruhusu Wamarekani kutoa sauti kwa hasira zao dhidi ya rais wa chama cha Democrat juu ya kuongezeka kwa vifo vya raia katika mashambulio ya Israeli kwenye Ukanda wa Gaza.

Wapiga kura huko New Hampshire watamchagua mgombea wanayempendelea katika kinyang'anyiro cha kuteua cha chama cha Democratic au Republican siku ya Jumanne lakini harakati hiyo wanaharakati wanaotaka kuarifu Ikulu ya White House mtazamo wa umma.

"Kwa muda wa miezi mitatu iliyopita, huku ulimwengu ukitazama ,vita vya Gaza vikiendelea kuwa mbaya, utawala wa Biden umekataa maombi yote ya kutaka kusitishwa kwa mapigano na kukomesha uungaji mkono wa Marekani kwa Israel," harakati hiyo imesema katika ujumbe kupitia X.

Vita vya maangamizi ya umati vya Israel dhidi ya Gaza hadi sasa vimepelekea Wapalestina wasiopungua 25,295 kupoteza maisha ambapo, karibu asilimia 70 kati yao wakiwa wanawake, watoto na vijana.

3486920

Habari zinazohusiana
captcha