IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Msikiti Uswidi wakabiliwa na hujuma kadhaa za chuki dhidi ya Uislamu

20:52 - February 23, 2024
Habari ID: 3478402
IQNA - Msikiti mmoja katika mji mkuu wa Uswidi wa Stockholm umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu kwa zaidi ya mwaka mmoja, huku tukio la hivi punde likitokea Jumatano wakati waumini wa Kiislamu walipoona ukuta wa msikiti ukiwa umechorwa Swastika ambayo ni nembo ya wanazi na maandishi ya "waue Waislamu "

Msikiti huo ulio jijini Stockholm katika wilaya ya Sodermalm umekumbwa na uhalifu wa chuki kwa mara ya pili wiki hii.

Ni moja tu ya vitisho na uhalifu wa chuki uliowalenga Waislamu katika mwaka uliopita.

Siku ya Jumanne, mhalifu pia alichora alama ya Swastika na ujumbe wa vitisho, akisema "nenda nyumbani" ulioandikwa kwenye mlango, wasimamizi wa msikiti huo ulisema kwenye chapisho kwenye tovuti yake.

Mohamed Amin, mjumbe wa kamati ya Msikiti wa Stockholm, aliiambia SVT TV kwamba "hivi karibuni tutalazimika kuweka chuma mbele ya madirisha ili kjilinda, kama katika gereza."

Wasimamizi wa msikiti pia walisambaza picha za madirisha yaliyovunjwa na wahalifu kabla ya kuondoka katika eneo la msikiti.

Wiki chache tu zilizopita, barua iliyokuwa na kitu kama unga ilitumwa msikitini, na bomu bandia pia liliripotiwa kuwekwa kwenye lango kuu.

Msikiti huo hapo awali ulikuwa ukilengwa na milango iliharibiwa mwezi Novemba.

"Vitisho kwa misikiti yetu lazima vichukuliwe kwa uzito zaidi," ilisema taarifa ya mkutano wa Jumuiya ya Kiislamu ya msikiti huo. Taarifa hiyo pia ililaani mashambulizi ya kibaguzi na kuzitaka mamlaka husika kuchukua hatua dhidi ya uhalifu wa chuki unaowalenga Waislamu.

Katika taarifa iliyotolewa kufuatia tukio la Jumanne, jumuiya hiyo iliwataka wanasiasa wa Uswidi kutanguliza mbele usalama wa jamii ya Kiislamu nchini humo, ikisema usalama wa Waislamu wa Uswidi kwa ujumla na hasa misikiti unahitaji kuwa juu zaidi katika ajenda ya kisiasa.

"Tunashuhudia taswira inayoongezeka ya vitisho dhidi ya misikiti na kimsingi inatokana na ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu ambao umepata nafasi katika mjadala wa vyombo vya habari na mazungumzo ya kisiasa.

"Ni wakati mwafaka wa kutoa kipaumbele kutatua uhalifu huu wa chuki ili tujisikie salama kufurahia uhuru wa kidini."

captcha