IQNA

Jinai dhidi ya Waislamu

Imamu wa Msikiti Marekani apigwa risasi na kuuawa

15:02 - January 04, 2024
Habari ID: 3478144
IQNA – Imamu wa msikiti mmoja New Ark, jimbo la New Jersey nchini Marekani, amepigwa risasi na kuuawa nje ya msikiti anakosalisha.

Imamu wa New Jersey amekufa baada ya kupigwa risasi nje ya msikiti wa Newark mapema Jumatano asubuhi, na mamlaka bado haijatambua mshukiwa au sababu ya shambulio hilo, waendesha mashtaka wa eneo hilo walisema.

Hadi sasa hakuna dalili kwamba ufyatuaji risasi huo ulikuwa uhalifu uliochochewa na chuki za kidini au ugaidi wa ndani ya nchi kulingana na ushahidi uliokusanywa hadi sasa katika uchunguzi, Mwanasheria Mkuu wa New Jersey Matthew Platkin amewaambia waandishi habari.

Ofisi ya Platkin haingeweza kutoa taarifa kamili  kwa sasa hasa kwa kuzingatia kuwa kuna ongezeko la hivi karibuni la matukio ya chuki dhidi ya wafuasi wa dini mbali mbali hasa Waislamu.

Imamu aliyeuawa siku ya Jumatano, Hassan Sharif, alipigwa risasi mara nyingi muda mfupi baada ya saa kumi na mbili asubuhi kwenye gari lake nje ya msikiti wa Masjid Muhammad huko Newark, alisema mwendesha mashtaka wa Kaunti ya Essex Theodore Stephens kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumatano. Sharif alifariki kutokana na majeraha yake katika hospitali ya eneo hilo Jumatano alasiri.

"Kuna wengi huko New Jersey hivi sasa ambao wanahisi hali ya hofu," Platkin alisema.

Matukio ya chuki dhidi ya Uislamu yameongezeka kote Marekani tangu kuanza kwa vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza mwezi Oktoba.

Mkurugenzi wa Usalama wa Umma wa New Jersey Fritz Frage aliunga mkono taarifa za Platkin na Stephens kwamba hakuna chochote hadi sasa ambacho kimeonyesha kwamba mpiga risasi alichochewa na chuki dhidi ya Uislamu, lakini akasema wachunguzi walikuwa wakifuata "maelekezo yote" wakiendelea kuchunguza tukio hilo.

3486679

Habari zinazohusiana
captcha