IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Jisajili Mashindano ya 17 ya Qur'ani Tukufu ya Al-Kawthar TV

17:56 - January 08, 2024
Habari ID: 3478168
IQNA - Usajili wa toleo la 17 la mashindano ya kila mwaka ya kimataifa ya Qur'ani yanayoandaliwa na Televisheni ya Al-Kawthar ulifunguliwa Jumatano iliyopita, sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Hazrat Zahra (SA).

Siku ya mwisho ya kujisajili ni  13 ya mwezi wa Rajab (Februari 25), ambayo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Ali (AS).

Wale walio tayari kujiandikisha kwa ajili ya shindano, wanaweza kurejelea kitengo maalumu kwenye tovuti rasmi ya Al-Kawthar TV ambayo ni  www.alkawthartv.ir 

Washiriki wanatakiwa kuwasilisha usomaji wa sauti, unaochukua dakika mbili hadi tatu wamojawapo ya sehemu zifuatazo za Qur'ani Tukufu:

      - Aya 161-165 za Surah Al-An'am

      - Aya 143-144 za Surah Al-A'raf

      - Aya 110-115 za Surah Hud

Washiriki bora tisini na sita, kulingana na tathmini za awali, watajulishwa juu ya kufuzu kwao kwa hatua inayofuata kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Washiriki wote tisini na sita waliochaguliwa wanatakiwa kupatikana kupitia Skype kwa vipindi vya matangazo ya moja kwa moja katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Uratibu huu utawezeshwa na timu ya utayarishaji ya Al-Kawthar TV.

Washiriki 24 watafuzu kwa nusu fainali. Kutakuwa na idadi isiyozidi ya washiriki wawili kutoka kila nchi, na hawa lazima wawe wasomaji bora kutoka mataifa yao.

Watazamaji watapata fursa ya kumpigia kura mshiriki mmoja zaidi ili afuzu kwa nusu fainali.

Hatimaye, washiriki watano bora kutoka nchi tano tofauti wataingia kwenye fainali kuu, iliyoratibiwa kuwa katika usiku uliobarikiwa wa Eid al-Fitr.

Washiriki wote, wenye umri wa miaka kumi na saba na zaidi, wanatakiwa waandike:

    - Majina yao kamili.

    - Nchi wanayoishi.

    - Umri .

    -  Nambari ya simu ya mawasiliano.

    - Hakikisha usomaji wao uliowasilishwa umeandikwa kwa uwazi sehemu iliyochaguliwa kwa mfano: Aya 143-144 za Surah Al-A'raf.

Kwa maswali na usaidizi wowote, wale wanaopenda kushiriki wanaweza kuwasiliana na kamati ya maandalizi kupitia WhatsApp kwa nambari +989108994025.

Mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu yanayofanyika kwa njia ya mawasiliano ya intaneti yamepewa anuani ya "Inna lil-Muttaqina Mafaza" (Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu- Quran Tukufu, Surat An Nabaa  aya ya 31)  na hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Ni mashindano makubwa zaidi ya ulimwengu ya Kiislamu ya usomaji wa Qur'ani moja kwa moja kwa njia ya televisheni yanayorushwa na Al-Kawthar, Televisheni ya lugha ya Kiarabu ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB).

3486728

 

Habari zinazohusiana
captcha