IQNA

Usajili wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Al Kauthar TV ya Iran waanza

21:21 - February 17, 2022
Habari ID: 3474938
TEHRAN (IQNA)-Usajili wa washiriki wa Awamu ya 15 ya Mashindano ya Kimataifa ya Kusoma Qur'ani Tukufu ya Televisheni ya Al Kauthar umeanza.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ambayo huandaliwa kila mwaka na Televisheni ya Al Kauthar yamepewa aya ya Qur’ani Tukufu isemayo إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا , "Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu".  (Qur’ani Tukufu 78:31).

Wale wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanaweza kujaza fomu kupitia tovuti ya https://mafaza.alkawthartv.ir/  au kuwasiliana na sekretariati ya mashindano kupitia nambari ya whatsapp ifuatayo +989108994025.

Wanaotaka kushiriki wanatakiwa kutuma klipu ya video ya dakika mbili inayowaonyesha wakisoma Qur'ani Tukufu.

4036880

Baada ya jopo la majaji kuchunguza klipi hizo, washiriki 96 waliofuzu watachaguliwa katika duru ya mchujo itakayorushwa mubashara katika Televisheni ya Al Kauthar kuanzia usiku wa kwanza hadi usiku wa 24 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Abbas Razavi, afisa mwandamizi katika Al Kauthar TV anasema usajili utaendelea hadi Machi 18 na kwamba majaji ni wataalamu wa Qur'ani kutoka nchi za Kiislamu duniani.

Al Kauthar ni Televisheni ya Kiarabu inayomilikiwa na Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB)

Mashindano ya mwaka jana yalikuwa na washiriki kutoka nchi 96 ambapo washinidi walikuwa ni kutoka Iran, Iraq na Indonesia.

 

captcha