IQNA

Tafsiri ya Qur'ani Tukufu

Ripoti inaangazia Ukosefu wa Tafsiri za Qur'ani Tukufu kuhusu saikolojia

18:52 - December 25, 2023
Habari ID: 3478088
IQNA - Ingawa kumekuwepo na juhudi nyingi za wanazuoni wa Kiislamu katika uwanja wa tafsiri ya Qur'ani Tukufu tangu kuja kwa Uislamu, kuna ukosefu wa kazi katika tafsiri ya kisaikolojia ya Kitabu Kitukufu.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya Televisheni ya Al Jazeera.

Taarifa hiyo imesema, tafsiri za Qur'ani Tukufu  tangu miaka ya mwanzo baada ya kuteremshwa kwa Kitabu kitukufu zimejikita zaidi katika nyanja za kiisimu, Fiqhi (kisheria) na kidini.

Hii ilisababisha utafiti muhimu na maendeleo ya ajabu katika isimu, mofolojia, na nyanja saw ana hizo.

Tafsiri hizo pia zimenufaika kutokana na nyanja mbalimbali za elimu kama vile historia. Lakini kumekuwa na ukosefu wa umakini kwa sayansi ya saikolojia.

Miaka iliyopita, Abdul Ghani al-Azhari, mwanazuoni mkuu wa Qur'ani Tukufu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar, aliandika makala tatu kuhusu tafsiri ya kisaikolojia ya Qur'ani Tukufu ambazo zilichapishwa na Jarida la Minbar al-Islam.

Hili lilimsukuma Mustafa Sadiq al-Rifaei, mwandishi mashuhuri wa Misri, kuandika kitabu juu ya vipengele vya miujiza ya kisaikolojia ya Qur'ani Tukufu.

Abdul Wahab Hamuda pia aligusia suala hili katika kitabu kiitwacho "Qurani na Saikolojia".

Baadaye Muhammad Othman Nijati aliandika kitabu chenye kichwa sawa. Kitabu cha Hamuda kinajadili tafsiri ya Qur'ani Tukufu kwa mtazamo wa kisaikolojia ambapo kazi ya Nijati ni tafsiri ya mada.

Mustafa Mahmoud ni mtaalamu mwingine wa Qur'ani Tukufu wa Misri anayefanya kazi katika uwanja huu. Aliandika kitabu kiitwacho "Saikolojia Mpya ya Qur'ani". Katika kitabu kingine, "Siri za Quran", alitenga sura moja kwa akili saikolojia ya Qur'ani.

Kazi nyingine ambayo tafsiri yake ya kisaikolojia inajadiliwa ni At-Tafsir al-Mawzuei Lil-Quran al-Kareem (tafsiri ya kimaudhui ya Quran) ya Mohamed al-Bihi. Alikuwa na ujuzi mzuri katika falsafa na saikolojia lakini alikufa kabla ya kukamilisha kazi hii.

Tafsiri ya Qur'ani Tukufu ya "Fi Zilal al-Quran" ( Katika Kivuli cha Qurani) ya  Sayyid Qutb bila shaka ni kazi muhimu zaidi katika zama za kisasa ambayo inakaribia tafasiri kisaikolojia ya Qur'ani Tukufu..

Licha ya juhudi hizo, kuna upungufu wa kazi za kufasiri ambapo aya zote za Qur'ani Tukufu ni darsa kwa mitazamo ya kisaikolojia.

4189675

Habari zinazohusiana
captcha