IQNA

Rais wa Ufaransa ashutumiwa kuwatesa Waislamu

23:08 - March 03, 2022
Habari ID: 3475001
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Ufaransa imeshutumiwa kwa kuwalenga Waislamu kwa njia iliyoratibiwa.

Ufaransa imeshutumiwa kwa kuwalenga Waislamu wa nchi hiyo kwa kufuata sera nyingi zilizoletwa na ofisi ya Rais Emmanuel Macron kushughulikia kile kinachoitwa " Misimamo ya Kiislamu na misimamo ya kujitenga ".

Ripoti mpya ya shirika la utetezi wa haki la Uingereza la Cage inaangazia matumizi ya Macron ya mamlaka ya kiutendaji kuunda sera ya  kulenga vikundi na taasisi za Kiislamu nchini Ufaransa katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Sera hizo, zilizoandaliwa mwaka wa 2017,  awali zililenga kuchunguza sababu zilizopelekea wapiganaji raia wa Ufaransa kutoka maeneo fulani ya nchi hiyo kuelekea Syria na Iraqi kujiunga na makundi ya kigaidi. Uchunguzi huo  ulibadilika na kuwa mradi wa nchi nzima unaolenga kushughulikia "mielekeo ya Kiislamu" na "Waislau kujiondoa kwa jamii" kote nchini.

Tangu wakati huo, Ufaransa imeanzisha msururu wa sheria zenye utata ambazo mashirika kadhaa ya haki za binadamu yameona kuwa ni za chuki dhidi ya Uislamu.

Shirika la kutetea haki la Cage  limesema sera ya kukandamiza Wislamu ilitumika kuhalalisha kufungwa kwa takriban misikiti kumi na mbili, mamia ya biashara na mashirika ya misaada yanayomilikiwa na Waislamu, na kunyakua mali ya mamilioni ya euro kwa sababu ya madai ya kukuza misimamo ya Kiislau.

Miongoni mwa mashirika yaliyofungwa kwa madai ya kuendeleza Uislamu ni pamoja na shirika la kutoa misaada la Waislamu wa Ufaransa Barakacity na Jumuiya isiyo ya faida ya  Collective Against Islamophobia in France (CCIF), ambayo ilikuwa inafuatilia mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu kote Ufaransa. Mashirika yote mawili yanasema tuhuduma dhidi yao hazina msingi.

Idriss Sihamedi, rais wa Barakacity, alisema sera za Macron ziliundwa ili kuwafanya Waislamu wa Ufaransa wafuate nyayo za serikali bila kuuliza chochote.

"Ufaransa imeamua kuwalenga viongozi wa jumuiya na imeweka kila aina ya shinikizo kwa watu wanaotaka kuwatetea Waislamu," Sihamedi alisema katika taarifa yake.

Cage ilitangaza ripoti hiyo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Paris siku ya Jumatano ambapo imetoa wito wa kufutwa sera zilizo dhidi ya Waislamu na Uislamu Ufaransa.

Rayan Freschi, mtafiti wa Cage na mwanasheria nchini Ufaransa ambaye alifanyia kazi ripoti hiyo, alisema inafichua jinsi sera ya Islamophobia au chuki dhidi ya Uislamu inatekelezwa kwa njia iliyoratibiwa serikalini.

"Miaka minne iliyopita, serikali ya Ufaransa ilianzisha sera ya siri na kali ya chuki dhidi ya Uislamu," Freschi alisema katika taarifa yake.

Ripoti hii inaangazia jinsi serikali ya Ufaransa imebomoa haraka misingi ya uhuru wa jamii ya Waislamu kupitia mateso yaliyoratibiwa, na kueneza hofu na wahka miongoni mwa jamii nzima ya kidini: kufungwa maeneo 718, ukaguzi mara 24,884 na uporaji wa euro milioni 46  za Waislamu. “Ni wakati wa acha uwindaji huu wa wachawi dhidi ya Waislamu," imesema ripoti hiyo.

3478025

Kishikizo: macron ufaransa waislamu
captcha