IQNA

Waislamu Ufaransa

UN yailaumu Ufaransa kwa kwabagua wanawake Waislamu

18:23 - August 04, 2022
Habari ID: 3475578
TEHRAN (IQNA) – Ufaransa ilimbagua mwanamke Mwislamu ambaye alizuiwa kuhudhuria mafunzo ya ufundi stadi katika shule ya umma akiwa amevalia hijabu yake, kamati ya Umoja wa Mataifa iliamua.

Mnamo 2010, Naima Mezhoud, ambaye sasa ana umri wa miaka 45, alipaswa kupata mafunzo kama msaidizi wa usimamizi katika kozi iliyofanyika katika shule ya serikali, ambapo wanafunzi wanakatazwa na sheria kuvaa hijabu. Alipofika, mwalimu mkuu wa shule hiyo katika viunga vya kaskazini mwa Paris alimzuia kuingia.

Miaka sita kabla, mwaka wa 2004, Ufaransa ilikuwa imepiga marufuku uvaaji wa hijabu na alama nyingine za kidini zinazoonekana katika shule za serikali na watoto wa shule. Mezhoud alisema kuwa kama mwanafunzi wa elimu ya juu, hakupaswa kulengwa na sheria.

"Kamati inahitimisha kuwa kukataa kumruhusu (Mezhoud) kushiriki katika mafunzo akiwa amevaa hijabu ni kitendo cha ubaguzi wa kijinsia na kidini," Kamati ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa iliamua, kulingana na waraka huo.

Wizara ya mambo ya ndani na wizara ya mambo ya nje Ufaransa haikujibu mara moja ombi la maoni.

Athari zinazowezekana za uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa hazikuwa wazi mara moja. Mtaalamu wa sheria za uhuru Nicolas Hervieu wa Taasisi ya Mafunzo ya Kisiasa ya Paris alisema kuwa kulingana na yaliyojiri miaka ya nyuma ni wazi kuwa Ufaransa itapuuza na kutozingatia uamuzi wa kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa.

Ufaransa ni nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya na  kwa miaka mingi, nchi hiyo imetekeleza sheria za kuwakandamiza Waislamu.

Baadhi ya vyama vya Waislamu na mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa sheria hizo zimewalenga Waislamu na kuwaondolea mbali ulinzi wa kidemokrasia na kuwaacha katika hatari ya kudhulumiwa.

Mezhoud aliwasiliana na Kamati ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa baada ya kushindwa msururu wa rufaa katika mahakama za Ufaransa.

Kamati hiyo ilisema Ufaransa imekiuka vifungu vya 18 na 26 vya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa kuhusu uhuru wa kidini.

Wakili wa Mezhoud, Sefen Guez Guez, amewaambia waandishi habari kwamba uamuzi huo unaonyesha kuwa taasisi za kimataifa za haki za binadamu zinakosoa sera za Ufaransa kuhusu Uislamu.

"Taasisi za Ufaransa zitalazimika kuzingatia uamuzi wa Umoja wa Mataifa," aliongeza.

Kwa nadharia, kufuatia uamuzi wa kamati ya Umoja wa Mataifa, Ufaransa sasa ina miezi sita ya kufidia kifedha Mezhoud na kumpa fursa ya kuchukua kozi ya ufundi ikiwa bado anaitaka. Nchi pia lazima ichukue hatua ili kuhakikisha ukiukaji kama huo wa sheria za kimataifa hautatokea tena.

3479980

Kishikizo: ufaransa waislamu hijabu
captcha