IQNA

Serikali ya Ufaransa yafunga msikiti mjini Cannes

13:20 - January 13, 2022
Habari ID: 3474802
TEHRAN (IQNA)- Ufaransa imeendeleza ukandamizaji wake wa Waislamu kwa kutangaza kufunga msikiti mmoja katika mji wa Cannes.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin ametangaza Jumatano kuwa, msikiti huo uliop katika mji wa Cannes ulio katika pwani pwani ya Bahari ya Mediterranean kusini mashariki mwa Ufaransa. Darmanin amedai kuwa wahubiri katika msikiti huo wametoa matamshi dhidi ya Mayahudi na kuunga mkono makundi yanayodaiwa kuwa na misimamo mikali ya kidini ambayo ni CCIFna BarakaCity.

Hatua hiyo imekuja baada ya msikiti mwingine kufungwa kaskazini mwa Ufaransa kutokana na kile ambacho kimedaiwa ni misimamo mikali ya imamu wa msikiti.

Wiki hii pia Serikali ya Ufaransa imevunja Baraza la Fiqhi la Waislamu wa Ufaransa (CFCM) ikiwa ni muendelezo wa sera zake za kuwakandamiza Waislamu.

Hivi karibuni  kamati maalumu ya Bunge la Kitaifa la Ufaransa iliidhinisha sheria ya 'thamani za jamhuri' ambazo zilipendekezwa na rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo kwa ajili ya kukabiliana na kile alichokitaja ni 'Uislamu wa wanaotaka kujitenga.'

Waziri wa Mambo ya Ndani Ufaransa amedai katika ukurasa wake wa Twitter kuwa sheria hiyo inalenga kulinda thamani za jamhuri sasa na siku za usoni.

Katika miezi ya hivi karibuni Ufaransa imeshadidisha mbinyo dhidi ya Waislamu nchini humo ambapo hata maduka ya Waislamu yanafungwa kwa visingizio mbali mbali.

Maafisa wa serikali za mitaa Ufaransa sasa wanatumia kila kisingizio kufunga biashara za Waislamu ikiwa ni katika kutekeleza sera jumla za Rais Emmanuel Macron ambaye ameanzimia kuwadhoofisha Waislamu nchini humo.

Ufaransa ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, kuna zaidi ya Waislamu milioni 5.7 Ufaransa ambao ni takribani asilimia 8.8 ya watu wote nchini humo.

3477352

captcha