IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Kikao cha mafunzo ya Qur'ani nchini Russia chafanyika Tehran

14:32 - March 25, 2024
Habari ID: 3478571
IQNA - Kongamano la kujadili masomo ya Qur'ani nchini Russia au Urusi limefanyika kama sehemu ya Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran.

Hujjatul Islam Seed Reza Moadab, mkuu wa kitivo cha theolojia cha Chuo Kikuu cha Qom, alihutubia kongamano hilo, ambalo liliandaliwa na Kituo cha Kimataifa cha Utafiti na Elimu cha Hauza (Seminari za Kiislamu).

Msomi huyo alibainisha kuwa Russia ina wakazi milioni 142, huku Ukristo wa Orthodox, Uislamu, Ubudha na Uyahudi ukiwa na idadi kubwa ya wafuasi nchini humo.

Alisema watu wa Russia kwa ujumla wanapendezwa na mambo ya kiroho na mafanikio ya dini nchini humo yatategemea utendaji kazi wa wahubiri wa  wenye uwezo.

Hujjatul Islam Moadab pia alikitaja Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Moscow, na kubainisha kuwa chuo hichi ni mjumbe wa Baraza la Vyuo Vikuu vya Kiislamu Ulimwenguni.

Alisema wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Moscow hujifunza Qur'ani, Tafsir (Tafsiri ya Qur'ani), sayansi ya Qur'ani, Hadith, Sira ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), maadili ya Kiislamu na Fiqh.

Pia wanasoma vitabu katika nyanja za falsafa, uchumi, saikolojia, sayansi ya elimu, historia ya Russia, nk, alisema.

Kulingana na Hujjatul Islam Moadab wengi wa wahitimu wa chuo kikuu sasa wanahudumu kama maimamu na mamufti nchini Russia na nchi zingine.

Kwingineko katika matamshi yake amesisitiza juu ya ulazima wa kuwafunza wanafunzi wenye vipaji vya seminari wanaojua vizuri lugha ya Kirusi na wanaoweza kuandika vitabu vya Qur'ani na vya Kiislamu kwa lugha ya Kirusi.

3487714

Habari zinazohusiana
captcha