IQNA

Harakati za Qur'ani

Wahifadhi wa Qur'ani Tukufu waenziwa Rafah

15:14 - February 16, 2024
Habari ID: 3478360
IQNA - Makumi ya watoto huko Rafah, kusini mwa Gaza, ambao wamehitimu katika mafunzo ya

Maafisa wa kambi ya Rafah inayohifadhi wakimbizi hao kutokana na mashambulizi ya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza walifanya hafla ya kuwaenzi watoto hao.

Zaidi ya wavulana na wasichana 40 walisifiwa katika hafla hiyo ya kuhifadhi Juzuu (sehemu) kadhaa za Qur’ani Tukufu, tovuti ya Arab21 iliripoti.

Iliandaliwa katika Shule ya Shifa Amru ya kambi hiyo ambayo inahifadhi maelfu ya wakimbizi.

Licha ya mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza ambayo yamesababisha vifo vya raia wengi na maelfu ya wengine kuyahama makaazi yao, lakini shughuli za Qur'ani zinaendelea katika eneo hilo lililozingirwa.

Huko Rafah, ambayo iko karibu na mpaka na Misri, familia zimejenga mahema ambamo watoto hujifunza Qur’ani pamoja na mafundisho na maadili ya Kiislamu.

Utawala wa Kizayuni ulianza kampeni yake ya kinyama ya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Ghaza tarehe 7 Oktoba. Zaidi ya Wapalestina 28,500 wengi wao wakiwa wanawake na watoto wameuawa na makumi ya maelfu kujeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu ya Israel.

4200005

Habari zinazohusiana
captcha