IQNA

Jinai za Israel

Indhari ya Umoja wa Mataifa kuhusu hujuma ya utawala wa Israel dhidi ya Rafah

19:16 - February 09, 2024
Habari ID: 3478326
IQNA-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limeonya kwamba mashambulizi ya utawala haramu wa Israel dhidi ya mji wa mpakani wa Rafah wenye msongamano mkubwa wa watu Gaza yatakuwa "kichocheo cha maafa."

Ikiwa imepita miezi minne ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza, vikosi vya jeshi la utawala huo katili vimezidisha mashambulizi ya anga katika eneo la kusini kabisa la Gaza, ambapo zaidi ya nusu ya wakazi milioni 2.4 wa eneo hilo wamekimbilia hifadhi.

Ndege za kivita za utawala wa Israel zilishambulia mji huo usiku wa Alhamisi na Ijumaa.

Takriban watoto watatu walikuwa miongoni mwa watu wanane waliouawa Ijumaa asubuhi katika mashambulizi ya kijeshi dhidi ya nyumba huko Rafah. Kulingana na Hilali Nyekundu ya Palestina watano kati ya waliouawa walikuwa watu wa familia moja.

Vikosi vya kijeshi vya utawala utendao jinai wa Israel vimeshashambulia kwa mabomu maeneo ambayo walikuwa wamewaelekeza Wapalestina "kutafuta usalama."

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema katika chapisho la X siku ya Ijumaa kwamba uvamizi wa Israeli huko Rafah "utaongeza kwa kasi kile ambacho tayari ni jinamizi la kibinadamu na matokeo yasiyoelezeka ya kikanda."

Mapema wiki hii ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura OCHA ilionya kuwa hatua yoyote ya utawala haramu wa Israel ya uvamizi wake kamili wa Gaza hadi katika mji wa kusini wa Rafah wenye msongamano mkubwa wa watu inaweza kutajwa kuwa ni uhalifu wa kivita ambao lazima uzuiwe kwa gharama yoyote.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Geneva Uswisi msemaji wa OCHA Jens Laerke amesema “Sisi kama Umoja wa Mataifa na Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa tunaweza kushuhudia na tunaweza kuweka wazi kile ambacho sheria inasema, "chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, ulipuaji wa mabomu katika maeneo yenye watu wengi unaweza kuwa uhalifu wa kivita.”

Tangu ilipoanza vita vyake  vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mapema Oktoba mwaka jana, watu milioni 1.9 -  yaani asilimia 85 ya wakazi wa Gaza - wamekimbia makazi yao. Mashambulizi ya Israel pia yameua takriban watu 28,000 kufikia sasa, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.

3487119

Habari zinazohusiana
captcha