IQNA

Jinai za Israel

Msikiti Wenye Miaka 800 waharibiwa katika hujuma ya Israel dhidi ya Gaza

11:26 - December 08, 2023
Habari ID: 3478005
GAZA (IQNA) - Msikiti wa kihistoria wa Othman bin Qashqar, ulioko katika Jiji la Kale la Gaza ulilipuliwa kwa mabomu yaliyodondoshwa na ndege za kivita za utawala haramu Israel siku ya Alhamisi, na kusababisha Wapalestina kadhaa kuuawa shahidi na uharibifu wa nyumba zilizo karibu, shirika rasmi la habari la Palestina WAFA liliripoti.

Msikiti huo ulijengwa mwaka wa 620 Hijria (1220 Miladia), na ni moja ya misikiti kongwe na maeneo ya kiakiolojia katika Ukanda wa Gaza.

Msikito huo mkongwe Uko katika kitongoji cha al-Zaytoun, mashariki mwa Mji wa Gaza, na uko jirani na Msikiti Mkuu wa Al-Omari, ambao pia uliharibiwa na ndege za kivita za Israel wakati wa vita vya sasa vya mauaji ya kimbari vilivyoanzishwa na Israel dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7.

Tangu kuanza kwa vita hivyo, ndege za kivita za Israel zimeharibu makumi ya majengo ya kale katika jaribio la makusudi la kulenga urithi wa kitamaduni wa Palestina.

Mji Mkongwe wa Gaza una maeneo kadhaa ya  kihistoria ikiwa niapamoja na Kanisa la St Philip the Evangelist Chapel na Kanisa la St Porphyrius.

Kanisa la St Porphyrius lililojengwa miaka 1,600  lililipuliwa na jeshi katili la Israel mwezi Oktoba, wakati Waislamu na Wakristo walikuwa wamekimbilia eneo hilo kupata hifadhi wakati wa vita.

Kanisa hilo, lililojengwa awali mwaka wa 425 Miladia na lilipewa jina la Mtakatifu Porphyrius, ni mahali pa kale zaidi pa ibada ya Kikristo huko Gaza.

Shambulio hilo la Israel liliharibu kumbi mbili zilizopakana na jengo la kanisa hilo na kusababisha vifo vya takriban watu 18 waliokuwa wakitafuta hifadhi kwenye uwanja wa kanisa hilo.

Kulingana na Wizara ya Utamaduni ya Palestina, ndege za kivita za utawala dhalimu wa Israel zimedondosha mabomu katika majumba manane ya makumbusho, ikiwa ni pamoja na Makumbusho ya Rafah, Makumbusho ya Al-Qarara, na Makumbusho ya Khan Yunis.

Nyumba tisa za uchapishaji na maktaba pia ziliharibiwa, pamoja na uharibifu kamili au sehemu wa angalau vituo 21 vya kitamaduni.

Sehemu nyingi za Jiji la Kale la Gaza pia zimeharibiwa, ikiwa ni pamoja na majengo 20 ya kihistoria, makanisa, misikiti, makumbusho, na maeneo ya akiolojia.

Utawala haramu wa Israel unalenga kwa makusudia maeneo yenye turathi za kale Gaza ili kusambaratisha utambulisho wa eneo hilo la Wapalestina.

Tangu Oktoba 7, Wapalestina wasiopungua 17,000 wameuawa, wengi wakiwa ni wanawake na watoto na zaidi ya 43,616 wamejeruhiwa, kulingana na Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza.

3486330

Habari zinazohusiana
captcha