IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Wasiwasi Ujerumani kuhusu kuongezeka ubaguzi dhidi ya Waislamu kutokana na vita vya Gaza

21:14 - November 07, 2023
Habari ID: 3477854
BERLIN (IQNA) - Ujerumani imeelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa matukio ya ubaguzi wa dhidi ya Waislamu nchini humo tangu kuanza kwa mzozo wa Gaza Oktoba 7.

Msemaji wa serikali Steffen Hebestreit, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin, alikemea vikali mashambulizi yoyote dhidi ya Waislamu, akisisitiza kwamba vitendo hivyo, vikichochewa na sababu za kidini au nyinginezo, havikubaliki kabisa.

"Karibu Waislamu milioni 5 nchini Ujerumani wana kila haki ya kulindwa," Hebestreit alisema Jumatatu.

Muungano wa Kupinga Chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu (CLAIM), wenye makao yake makuu mjini Berlin, ulitoa onyo wiki iliyopita kuhusu kukithiri kwa ubaguzi dhidi ya Waislamu huku mzozo kati ya utawala wa kikoloni wa Israel na Palestina ukishadidi katika Ukanda wa Gaza.

Rima Hanano, mkuu wa shirika hilo lisilo la kiserikali, alielezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu kushadidi ubaguzi dhidi ya Waislamu nchini Ujerumani, akisisitiza haja ya kulichukulia suala hili kwa uzito wake.

Muungano wa Kupinga Chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu Umerekodi visa 53 vya vitisho dhidi ya Waislamu, ghasia na ubaguzi katika muda wa wiki mbili na nusu zilizopita, ikiwa ni pamoja na mashambulizi 10 dhidi ya misikiti.

Inakisiwa kuwa idadi kubwa ya matukio ambayo hayajaripotiwa ya chuki dhidi ya Uislamu bado hayajasajiliwaa, yakiwemo matukio ya matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu kwenye mitandao ya kijamii.

CLAIM imetoa wito wa kuchukuliwa hatua za kina ili kukabiliana na ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu na kuhakikisha ulinzi wa wale walioathirika. Shirika hilo limesisitiza udharura wa kuchukuliwa hatua dhidi ya ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya Waislamu na aina nyinginezo za itikadi potofu kwa ajili ya demokrasia na mafungamano ya kijamii.

Kwa kuzingatia matukio hayo, Ujerumani inahimizwa kushughulikia na kupambana na suala linaloibuka la ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu na kuchukua hatua za kuhakikisha usalama na ustawi wa raia wake Waislamu.

3485912

Habari zinazohusiana
Kishikizo: waislamu ujerumani
captcha