Dua hizi za kila siku za Mwezi wa Ramadhani husomwa toka mwanzo ya tarehe mosi Ramadhani hadi siku ya mwisho katika mwezi huu mtukufu. Kila dua ina siku yake, na inaweza kusomwa mara nyingi kadiri ya uwezo wa mtu mwenyewe.
Ee Mwenyezi Mungu! Nioneshe njia ya kuifikia Radhi yako, wala Usimpe Shetani nafasi ya kunihangaisha katika mwezi huu. Uijaalie Pepo iwe ndiyo mashukio yangu na mapumziko. Ewe Mwenye kuzitekeleza haja za wakuombao.