Ee Mwenyezi Mungu! Nizindushe katika mwezi huu ili nipate baraka za masiku yake, Uninawirishe moyo wangu kwa mwangaza wa nuru zake (Nuru za mwezi huu wa Ramadhani) Uvishike viungo vyangu vyote viwe ni vyenye kufuata nyayo zake, kwa Nuru yako ewe Mwangaza wa nyoyo za wakujuao.