IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran

Qari wa Qur’ani kutoka Kenya: Mashindano ya Qur’ani ya Iran yalikuwa magumu

21:57 - February 24, 2023
Habari ID: 3476603
TEHRAN (IQNA) - Ustadh Muhammad Ahmad Mohammad Mohiuddin, Qari wa Qur’ani Tukufu kutoka Kenya alikuwa miongoni mwa washiriki katika Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyofanyika kuanzia Februari 18-22.

Katika mahojiano na  katika mahojiano na IQNA, amesema mashindano hayo yalikuwa magumu na pia amempongeza mwalimu wake nchini Kenya, Ustadh Haitham Sagar Ahmad kwa kumuwezesha kufika katika kiwango cha kushiriki mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu. Hapa chini ni mahojiano yake na IQNA. 

Duru hii ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ilifanyika katika hatua mbili, ambapo duru ya kwanza ilifanyika kwa njia ya intaneti miezi kadhaa iliyopita na kushirikisha wagombea 150 kutoka nchi 80.

Kutoka miongoni mwao, maqari wa Qur'ani na waliohifadhi Qur'ani kutoka nchi 33 walifika kwenye fainali iliyofanyika mjini Tehran Februari 18-22. Mashindano hayo yalifunguliwa sambamba na mnasaba wa kukumbuka Kubaathiwa au kupewa utume, Mtume Muhammad SAW.

Kauli mbiu ya mashindano ya mwaka huu, kama lile lililotangulia, ni "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja", jambo ambalo linaashiria Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipa umuhimu mkubwa umoja na udugu kati ya mataifa ya Kiislamu.

Shirika la Wakfu na Misaada la Iran kila mwaka huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa kushirikisha wanaharakati wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbalimbali.

captcha