IQNA

Muhtasairi kuhusu Tafsiri na Wafasiri wa Qur'ani Tukufu/1

Utangulizi wa Tafsiri na Wafasiri wa Qur'ani Tukufu/1

21:26 - September 04, 2022
Habari ID: 3475733
TEHRAN (IQNA) – Tafsir (tafsiri) ni istilahi katika sayansi ya Kiislamu ambayo ina maana ya kueleza maana ya aya za Qur'an Tukufu na kutoa mafundisho kutoka kwayo.

Sayansi ya Tafsiri, ambayo somo lake ni tafsiri, ni moja ya nyanja pana katika sayansi ya Kiislamu.

Tafsiri inatokana na mzizi wa neno Fisr, ambalo katika lugha za Kisemiti linamaanisha kuyeyusha kitu na katika matumizi ya baadaye pia ilitumika katika maana ya tafsiri ya ndoto.

Kuna sitiari katika maana hii kwani inafanananisha tafsiri na kuyeyusha madini ili kupata vito vya thamani.

Isipokuwa Muqatta'at (mchanganyiko wa herufi baina ya herufi moja hadi tano inayoonekana mwanzoni mwa sura 29 kati ya sura 114 za Qur'ani), aya za Qur'ani ni za namna ambayo zinaleta maana ya kwanza wakati wa kuzisoma. Kinachoitwa Tafsir ni matokeo ya elimu au ujuzi unaovuka ujuzi wa kawaida wa lugha.

Mfano wa kwanza wa kazi zinazojulikana kama Tafsir al-Qur'an ulianzia karne ya 8 Hijria (kati ya 750 na 770 Miladia). Kazi hizo ni pamoja na mchanganyiko wa mitazamo ya tafsiri za Masahabah wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW)) na Tabiun (kizazi cha Waislamu waliofuata masahaba). Waandishi wa Tafsiri walijumuisha maoni yao katika uga wa tafsiri.

Kazi kama hizo , Tafisr al Qur'an ziliandikwa huko Iraq, Makka na Khorasan ( eneo la sasa lakaskazini-mashariki mwa Iran). Katika maeneo mengine  mengine ambayokama vile Sham na Madina, iliwachukua Mufaseer (wafasiri) muda mrefu zaidi kuandika vitabu vya Tafsiir.

Baada ya kuanzishwa kwa vyuo vikuu vya Kiislamu kama vile cha cha Al-Azhar, Nizamiyah, na nyinginezo, katika karne ya 10 na 11, maendeleo makubwa yalitokea katika elimu ya kidini. Vyuo vikuu vya Kiislamu na shule za Kiislamu zilifundisha sayansi tofauti na kufafanua upya hadhi na jukumu la  kila sayansi.

Waandishi wa vitabu vya Tafsir wakati huo walikuwa wasomi katika nyanja mbalimbali za elimu. Walijumuisha wataalamu wa mambo ya juu, Faqihi (mafaqihi), wanazuoni wa Hadith, na wanazuoni wa fasihi. Hii ni dalili kwamba waliamini mtazamo wa upande mmoja katika tafsiri ya Qur'ani unapaswa kuachwa na nyanja mbalimbali za elimu zitumike katika tafsiri ya Qur'ani.

Ndio maana uhusiano baina ya Tafsir na nyanja nyinginezo kama vile theolojia na Fiqh ukawa na muhimu sana kuanzia karne ya 12 na Tafsir ikajulikana kama fani inayojitegemea ya elimu inayotumia mafanikio ya nyanja nyinginezo.

Karne hiyo ya 12 ni ile ambayo wafasiri wa Qur'ani Tukufu walijaribu kupanga misingi ya tafsiri, kuweka ndani mafanikio ya nyanja nyinginezo na kuzitumia katika muundo jumuishi na ulioratibiwa.

Hatua za kwanza katika njia hiyo ni pamoja na kuandika utangulizi mfupi au mrefu wa wafasiri katika vitabu vyao vya Tafsirr. Katika utangulizi huo, walitaja mada ambazo zilikuwa aina ya masomo ambayo baadaye yalijulikana kama sayansi ya Qur'ani.

captcha