IQNA

Sura za Qur’ani Tukufu /27

Mazungumzo ya Nabii Sulaiman na Wanyama katika Surah An-Naml

19:11 - August 26, 2022
Habari ID: 3475684
TEHRAN (IQNA) – Nabii Sulaiman (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-AS-) alikuwa Mtume pekee wa Mwenyezi Mungu ambaye pia alikuwa mfalme na alikuwa na elimu na mali nyingi. Pia alikuwa na uwezo wa kuzungumza na wanyama na alikuwa na jeshi kubwa la watu na majini ambalo lilimpa nguvu zisizo za kawaida.

Sura ya 27 ya Qur’ani Tukufu inaitwa Surah An-Naml. Ni Sura ya 48 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Surah An-Naml ni Makki, ina aya 93 na iko katika Juzuu za 19 na 20 za Qur’ani Tukufu.

Naml ina maana ya mchwa kwa Kiarabu na Sura ina jina hili kwa sababu sehemu yake inahusu mazungumzo kati ya Nabii Sulaiman (AS) na wadudu chungu. Katika Sura An-Naml aya ya 17-19 tunasoma hivi: “Na alikusanyiwa Sulaiman majeshi yake ya majini, na watu, na ndege; nayo yakapangwa kwa nidhamu.  Mpaka walipo fika kwenye bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu mmoja: Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Sulaiman na majeshi yake bila ya wao kutambua.  Basi (Sulaiman) akatabasamu akacheka kwa neno hili, na akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema”. 

 

Katika Sura hii, Mwenyezi Mungu anarejea hadithi za Manabii watano, ambao ni Musa (AS), Daud (Daud), Sulaiman (AS), Saleh (AS) na Lut (AS), wakiwapa habari njema waumini na kuwaonya makafiri.

Sura pia inajumuisha mijadala kuhusu Tauhidi na kile kinachotokea Siku ya Kiyama.

Ni sura ya pekee katika Quran Tukufu ambayo ndani yake kuna Bismillah Ar-Rahman Ar-Rahim (Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu).

Mojawapo inakuja mwanzoni mwa Sura kama Sura zingine na nyingine mwanzoni mwa barua ambayo Sulaiman (AS) alimuandikia Belqis, Malkia wa Saba (Sheba), ambayo iko katika aya ya 30.

Kwa mujibu wa Allamah Tabatabai, mfasiri maarufu wa Qur’ani aliyeandika Tafisri ya Al Mizan, lengo kuu la sura hii ni kutoa habari njema kwa waumini na kuwaonya makafiri). Ndiyo maana inataja kwa ufupi hadithi za idadi kadhaa ya Mitume wa Mungu.

Sura pia inaelekeza kwenye elimu ya Mungu isiyo na kikomo na ukuu wake juu ya ulimwengu wote.

Surah An-Naml inasimulia hadithi za Daud (AS) na Sulaiman (AS) kwa undani.

Hadithi za kuelimishana zinazungumzia masuala mbalimbali kama vile elimu ya Daud (AS) na Sulaiman (AS), uwezo wa Sulaiman (AS) kuzungumza na ndege na wanyama wengine, hatua yake ya kuunda jeshi la watu na majini, mazungumzo yake na wadudu chungu, kisa cha ndege aitwaye Hududu (mjumbe wa Mtume Sulaiman), kurejea kwa Hudhud na ripoti yake kuhusu Malkia wa Sheba, barua ya Sulaiman (AS) kwa Malkia wa Shebq, na ziara yake kwenye kasri ya Sulaiman (AS) na kuwa kwake muumini.

“Na akawakagua ndege, na akasema: Imekuwaje, mbona simwoni Hudhud, au amekuwa miongoni mwa walio ghibu?  Kwa yakini nitamuadhibu kwa adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja ya kutosha.  Basi (Hudhud) akakaa si mbali na akasema: Nimegundua usilo gundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea khabari za yakini.  Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa. (An –Naml 20-23)

Habari zinazohusiana
captcha