Maonyesho hayo yaliyopewa jina la “Maonyesho ya Kitaifa ya Misahafu na Miradi ya Wajasirimali Wadogo” yanafanyika kwa ushirikiano na Baraza la Wazazi katika sherehe iliyodhuhuriwa na Sheikh Haitham bin Saqr al Qasimi, naibu mkuu wa ofisi ya mtawala wa Sharjah eneo la Kalba.
Dkt. Ali Obaid, Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sharjah amesema idadi kubwa ya idara za serikali na sekta binafsi zimeshiriki katika maonyesho hayo. Imedokezwa kuwa maonyesho haya yana vibanda 45 vya miradi mbali mbali ya sanaa za mikono na Misahafu.