Kwa mujibu wa taarifa Msahafu huo wa aina yake umeandikwa kwenye turubai na maandishi yameandikwa kwa aluminiumu na dhahabu. Aidha inaaminika kuwa ni msahafu wa aina yake katika historia ya Uislamu.
Kazi hii ni ya Mpakistani ambaye ameamua kuweka historia kwa kuandika aya za Qur'ani Tukufu kwa njia maalumu kwa mara ya kwanza. Shahid Rassam alianzisha mradi wake huo miaka mitano iliyopita na amepata zawadi kadhaa za kimataifa kutokana na mradi wake huo na hivyo anatazamia kuonyesha kazi yake hiyo katika maonyesho hayo ya kimataifa ya Dubai yatakayoanza Oktoba 20 na kuendelea kwa miezi sita.
Msahafu huo una urefu wa futi 8.5 na upana wa futi 6.5 na una jumla ya kurasa 550.