IQNA

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani Uturuki wazawadiwa

18:34 - June 18, 2016
Habari ID: 3470394
Sherehe za kufunga Mashindano ya 4 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Uturuki zimefanyika Ijumaa hii mjini Istanbul.

Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na Rais Recep Tayyip Erdogan, washindi wa kategoria za kuhifadi na kusoma waltangaza na kutunukiwa zawadi.

Jopo la majaji liliwatangaza wawakilishi wa Indonesia, Ufilipino na Bahrain kuwa walishika nafasi za kwanza hadi tatu kwa taratibu huku qarii kutoka Iran, Mehdi Ghulamnejad akipata nafasi ya nne.

Katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, hafidh kutoka Bangladesh alipata nafasi ya kwanza akifuatiwa na wawakilisho wa Tajikistan, Somalia na Palestina.

Hafidh kutoka Iran, Saeed Aliakbari hakuwa miongoni mwa washindi ingawa wengi walitaraji atangazwe miongoni mwa tatu bora kutokana na ustadi wake.

Mashindano ya Nne ya Kimataifa ya Qur'ani yalifunguliwa rasmi Juni 11 katika Msikiti wa Fateh mjini Istanbul.

Mashindano ya mwaka huu yalikuwa na washiriki 89 wasomaji (quraa) na waliohifadhi Qur'ani (hufadh) kutoka nchi 55.

Mashindano hayo huandaliwa na Idara ya Masuala ya Kidini ya Uturuki katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wanaoandaa mashindano hayo wanasema lengo ni kustawisha utamaduni wa Qur'ani na kuhimiza usomaji na kuhifadhi Kitabu hicho Kitakatifu. Jopo la majaji katika mashindano ya mwaka hii ni wataalamu wa Qur'ani kutoka Uturuki, Malaysia, Saudi Arabia, Morocco, Lebanon na Somalia.

3460119

captcha