IQNA

Wabangladesh wapinga kufutwa Uislamu kama dini rasmi

15:31 - March 26, 2016
Habari ID: 3470216
Maelfu ya Wabangladesh wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo kupinga njama za kutaka Uislamu usitambuliwe kuwa dini rasmi ya nchi hiyo.

Habari zinasema kuwa, wananchi zaidi ya elfu 3 waliandamana jana nje ya Msikiti wa Jamia wa jijini Dhaka baada ya Swala ya Ijumaa, kulaani azma wanayosema kuwa inakiuka sheria na katiba ya nchi ya kuitaka Mahakama Kuu nchini humo itangaze kuwa Uislamu sio dini rasmi ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, pendekezo hilo liliwasilishwa mahakamani na kundi la wananchi wanaojiita mashahuri nchini humo.

Azma hiyo ya kutaka kuifuta dini tukufu ya Kiislamu kuwa dini rasmi ya nchi hiyo inafanyika katika hali ambayo, zaidi ya asilimia 90 ya wananchi milioni 160 wa Bangaldesh ni Waislamu.

Licha ya kiongozi wa zamani wa kijeshi nchini humo H.M Ershad kutangaza Uislamu kuwa dini rasmi nchini Bangaldesh mwaka 1988, lakini Waziri Mkuu wa sasa Sheikh Hasina alitumia usekulari kama nguzo ya katiba ya nchi hiyo mwaka 2011. Hata hivyo Uislamu ulibakia kuwa dini rasmi ya taifa.

3484525

captcha