IQNA

Jinai za Israel

Walowezi wa Kizayuni washadidisha hujuma dhidi ya matukufu Kikristo huko Palestina

19:06 - July 24, 2023
Habari ID: 3477330
AL-QUDS (IQNA) - Mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya matukufu ya Kikristo na makanisa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel yamekuwa yakiongezeka katika miezi ya hivi karibuni

Tukio la hivi punde lilikuwa shambulio kwenye Jumba la watawa la Mar Elias na Kanisa huko Haifa wakati kuhani mkuu Padre Samer Zaknoun alipokuwa akihojiwa na tovuti ya habari ya Safa.

Zaknoun alikuwa kwenye simu na mwandishi wa habari wa Safa kuzungumzia wimbi la hivi punde la mashambulizi dhidi ya maeneo matakatifu ya Kikristo nchini Israel na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, wakati kundi la Walowezi wa Kiyahudi lilipovamia kinyama jumba hilo la watawa na kushambulia kanisa na waumini. Shambulio hilo lilikuwa la tano la aina yake. Ilianza na idadi ndogo ya walowezi, na kisha likageuka kuwa shambulio kubwa.

Shambulio hilo lilitanguliwa na wengine dhidi ya Kanisa la Maronite huko Acre na nyumba ya watawa huko Jaffa, ambapo walowezi wa Kizayuni walijaribu kuchukua udhibiti na kufanya ibada zao za Talmudi ndani yake, wakidai - kwa uwongo, - kwamba eneo hilo lina makaburi ya makuhani wa Kiyahudi.

Kuongezeka kwa mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Wakristo kunachukua mkondo hatari ambapo kumekuwa na angalau mashambulizi 40 yaliyorekodiwa katika miezi michache iliyopita.

Padre Zaknoun ameliambia shirika la habari la Safa kwamba Makanisa ya Kikristo yamekuwa yakilengwa kila siku na magenge ya walowezi, ambao ni wazi wanatumia fursa ya msimamo mkali unaoonyeshwa na uongozi wa kisiasa wa Israel dhidi ya Waislamu na Wakristo.

Ameonya kuwa kushindwa kwa utawala wa Israel kuyazuia makundi hayo ya Kizayuni kunawatia moyo kutumia hali hiyo na kuzidisha mashambulizi yao na hivyo kufifisha uwepo wa Wakristo huko Palestina.

Walowezi wote wa Kizayuni wamepora ardhi za Palestina na kujenga makazi yao kinyume cha sheria a za kimataifa. Utawala haramu wa Israel unadharau waziwazi sheria za kimataifa kutokana na uungaji mkono unaopata kutoka kwa madola ya Magharibi hasa Marekani.

Habari zinazohusiana
captcha