Maafisa wengine kadhaa kutoka pande hizo mbili pia walikuwepo kwenye mkutano huo. Vyombo vya habari vya Iraq vimeelezea mkutano huo wa Jumatatu asubuhi kama wa kufurahisha. Akiongoza ujumbe wa ngazi za juu, Ayatullah Al-Hakim amesafiri hadi mji mkuu wa Misri kwa mazungumzo na maafisa wa nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika. Ujumbe wa Iraq pia ulikutana na rais na waziri wa mambo ya nje wa Misri siku ya Jumapili.
Wakati wa mazungumzo hayo, Ayatullah Al-Hakim alisisitiza haja ya kudumisha mwelekeo chanya wa sasa wa mahusiano ya kikanda ili kuimarisha usalama na utulivu wa kikanda. Pia alionya kuhusu changamoto ambazo mkoa huo utakabiliana nazo endapo hali hii itadhoofika.
4144387