IQNA

Wanasiasa Waislamu

Meya wa Kwanza Muislamu achaguliwa Johannesburg Afrika Kusini

21:28 - February 07, 2023
Habari ID: 3476528
TEHRAN (IQNA)- Kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Kusini, diwani Muislamu kutoka chama kidogo cha Al Jama-ah amechagualiwa kuwa Meya wa Jiji la Johannesburg, kitovu cha biashara cha nchi hiyo.

Thapelo Amad, amepigiwa kura na baraza la jiji kuchukua nafasi ya meya Mpho Phalatse, mwanachama wa chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini, Democratic Alliance (DA).

Baada ya kuchaguliwa, Amad mwenye umri wa miaka 41 amesema, uteuzi huo umemzidi na kumpa unyenyekevu kwa kuwa Muislamu wa kwanza kuongoza jiji kubwa la nchi hiyo.

"Inaashiria historia nchini Afrika Kusini," ameliambia baraza hilo la Jiji la Johannesburg baada ya upigaji kura.

Meya huyo mpya ameahidi kuvifanya vita dhidi ya ufisadi kipaumbele chake kikuu.

Amad amechaguliwa kwa kuungwa mkono na chama tawala cha African National Congress (ANC), ambacho kinashikilia viti vingi zaidi katika baraza hilo ingawa alikosa kupata wingi wa kura katika uchaguzi wa 2021 wa jiji hilo kuu la kibiashara la Afrika Kusini.

Mtangulizi wake, Bi Phalatse mwenye umri wa miaka 45, aliondolewa kwa kura ya kutokuwa na imani naye mapema wiki hii.

Phalatse alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuongoza kituo hicho kikuu cha uchumi cha Afrika Kusini mnamo 2021, baada ya ANC kushindwa katika chaguzi za serikali za mitaa katika matokeo mabaya zaidi ya uchaguzi kiliopata tangu kurasimishwa demokrasia nchini humo mwaka 1994.

4117931

captcha