Akaunti hiyo, inayojulikana kama Al-Mushaf, kwa kawaida husambaza aya za Quran Tukufu na ina idadi kubwa zaidi ya wafuasi kati ya akaunti za Qur’ani Tukufu kwenye Twitter.
Hatua hiyo dhidi ya Al-Mushaf imeibua hasira miongoni mwa Waislamu wengi wanaoichukulia hatua hiyo kuwa ya kibaguzi.
Wanasema Twitter inapuuza kwa urahisi maudhui ya chuki, vurugu na uasherati lakini inasitisha akaunti inayotuma aya za Qur’ani
Wanashangaa jinsi kutwiti aya za Quran kunaweza kukiuka miongozo ya Twitter.
Mtumiaji wa Twitter alisema mtandao huo wa kijamii una matatizo na Uislamu lakini hauna matatizo na wasiomumini Mungu Mmoja na uasherati.
4120045