Bibi Maryam, mama yake Nabii Isa au Yesu ametajwa katika Qur'ani Tukufu kuwa ni mwanamke mwema, ambaye hakuwa mtume bali alilelewa kama mtume na ambaye mwenendo wake ulikuwa kama ule wa mitume wa Mwenyezi Mungu.
Qari wa Iraq, Hassan al-Zabhawi, alisoma aya ya 37 ya Sura Al Imran, ambayo inazungumzia kuhusu riziki ya Mwenyezi Mungu aliyopelekewa Bibi Maryam.
"Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu."