Watu kutoka kijiji alikozaliwa cha Kifr al-Mahrouq na vijiji na miji ya karibu pia walishiriki katika mazishi hayo, yaliyofanyika Jumanne baada ya sala ya adhuhuri.
Kulingana na wanakijiji, alikuwa Hafidh wa Qur'ani mwenye umri wa juu katika jimbo hilo. Watu wengi wa kijiji hicho na wale kutoka sehemu nyingine za mkoa walijifunza na kuhifadhi Qur'ani chini yake.
Quran Tukufu ndiyo maandiko pekee ya kidini ambayo yanahifadhiwa kikamilifu na wafuasi wake ambapo waliohifadhi huweza kusoma aya zote bila kutizama maandishi.
Watu wasiohesabika katika kila umma wa Kiislamu wamehifadhi Quran tangu siku ya kwanza ilipoteremshwa.
Qur'ani Tukufu ina Juzuu (sehemu) 30, Sura 114 (sura) na aya 6,236.
4103529