IQNA

Jeshi la Israel labomoa misikiti, mahospitali Ghaza

10:12 - August 03, 2014
Habari ID: 1435255
Utawala wa Kizayuni wa Israel haujatosheka kwa kuwaua kwa umati wanawake na watoto wa Ghaza bali pia umeharibu kwa mabomu idadi kubwa ya misikiti na mahospitali katika ardhi hiyo ya Wapalestina.

Kanali ya Televisheni ya Al Mayadeen imeripoti kuwa katika hujuma ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza mahospitali na vituo vya afya 44 vimeharibiwa kabisa. Hivi sasa aghalabu ya Wapalestina waliojeruihiwa katika vita vya Ghaza hawana sehemu za kupata matibabu.  Mbali na kubomoa mahospitali, jeshi la Kizayuni pia limeharibu kabisa misikiti 41 katika Ukanda wa Ghaza. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jeshi la utawala haramu wa Israel limeshambulia na kubomoa misikiti hiyo ambayo ilikuwa sehemu ya hifadhi ya Wapalestina ambao nyumba  zao zimeharibiwa kwa mabomu.
1435230

Kishikizo: ghaza israel hama misikiti
captcha