IQNA – Baraza Kuu la Fatwa la Syria limesema mojawapo ya kanuni zisizopingika za Uislamu ni marufuku ya usaliti na kushirikiana na adui Mzayuni au Muisraeli ambaye ni mwovu na mhalifu.
IQNA-Maandamano ya watu karibu milioni moja yamefanyika huko Sanaa, mji mkuu wa Yemen, jana Ijumaa katika kutangaza mshikamano wao na Wapalestina huko Gaza na kulaani uchokozi wa jeshi la Israel huko Gaza na Yemen.
IQNA – Idara inayosimamia kaburi au Haram ya Hadhrat Abbas (AS) huko Karbala, Iraq imetangaza usambazaji wa takriban nakala 15,000 za Qur’ani Tukufu na vitabu vya sala kwa ajili ya matumizi ya mamilioni ya waumini wanaotembelea eneo hilo takatifu.
IQNA – Karibu watu milioni mbili waliswali katika Al-Rawdah Al-Sharif ndani ya Al Masjid An Nabawi (Msikiti wa Mtume) huko Madina wakati wa msimu wa Hija wa mwaka uliopita wa 1446 Hijria.