IQNA

Sanaa katika Uislamu

Msanii anaonya kuhusu kufifia kaligrafia ya Qur'ani

16:01 - April 21, 2024
Habari ID: 3478710
IQNA - Mwandishi kaligrafia nchini Iran ambaye ni mtaalamu wa uandishi wa maandishi ya kidini, hususan aya za Qur'ani Tukufu, amebainisha wasiwasi kuhusu kupungua kwa idadi ya watu wanaojifunza kaligrafia ya Qur'ani.

Akizungumza na IQNA, Hujjatul Islam Abdollah Abdollahzadeh alisema kwamba alianza safari yake kwa kutumia kaligrafia mwaka 1989 na hivi karibuni akafikia kiwango cha mwandiko ambacho walimu wake waliona kuwa kinakubalika.

"Aya za Qur'an zilizoandikwa kwa maandishi ya Naskh zilinivutia," msanii huyo wa Qom alisema, akibainisha kwamba hamu hiyo ya kina ilimfanya ajishughulishe na kuandika Qur'ani, na pia hadithi za Ahlul al-Bayt (AS).

Kwa wale wanaotaka kuandika aya za Qur'ani, ujuzi wa maandishi ya Nashq au Thuluth ni muhimu, alisisitiza. "Kwa miaka mitatu ya mazoezi ya bidii, niliboresha ujuzi wangu katika maandishi ya Naskh na kuandika aya za Qur'ani Tukufu kwa mara ya kwanza mnamo 1992."

Katika nyakati za kisasa, maandishi ya maandishi na uandishi wa aya za Qur'ani Tukufu mara nyingi huonekana zaidi kama "sanaa ya mapambo badala ya taaluma ya msingi," Abdullahzadeh alisema, akiongeza kwamba ujio wa uchapishaji wa haraka na wa kisasa umefanya kazi zilizoandikwa kwa mikono kuwa kuoenekana kama zisizohitajika  baada ya kutokana na gharama zao za juu.

Wakati waandishi wa kaligrafia bado wamepewa kazi ya kuandika Misahafu katika maeneo kama Saudi Arabia na, kwa kiasi kidogo, Iran, ufundi huo hauheshimiwi kama ilivyokuwa hapo awali, amebainisha kwa masikitikko

Kadiri teknolojia na ulimwengu wa kidijitali inavyosonga mbele, kumekuwa na upungufu mkubwa wa wanafunzi wanaofuata uandishi wa kaligrafia, mwanazuoni huyo wa Kiisalmu amebaini.

Artist Warns of Waning Tradition of Quranic Calligraphy

Katika moja ya wilaya za Qom ambayo ni makazi ya takriban watu 400,000, kuna darasa moja tu la lenye wanafunzi 10 wanaojifunza kaligrafia ikkiwa ni idadi ndogo ya kushangaza kwa eneo hilo lenye watu wengi, alibainisha.

Kaligrafia ni sanaa ya gharama kubwa na huchukua muda mwingi, jambo ambalo linaweza kuwa moja ya sababu ya kupungua kwa wanaojishughulisha na aina hii ya sanaa alisema, akibainisha, "ili kuwatia moyo vijana wa kisasa kukumbatia sanaa hii, lazima kwanza tutambue na kuwaheshimu wasanii wa sasa katika uwanja huu."

3488024

captcha