IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu /35

Mfasiri wa kwanza wa Qur'ani Tukufu kwa Kichina

14:10 - November 26, 2023
Habari ID: 3477951
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Ilyas Wang Jingzhai (180-1949) ndiye mtu wa kwanza aliyetafsiri Qur'ani Tukufu nzima katika lugha ya Kichina.

Jingchai alizaliwa huko Tianjin kaskazini-mashariki mwa China katika familia ambayo kulikuwa na wasomi wengi wa kidini.

Babu na baba yake walikuwa miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu wa China na mama yake pia alikuwa mtu msomi katika sayansi ya Kiislamu.

Jingchai alisoma sayansi ya Kiislamu na kuanza shughuli za kueneza dini baada ya kuhitimu mwaka wa 1905.

Mnamo 1922, alisafiri kwenda Misri na kuingia Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar. Kisha alitembelea Makka na baada ya kutekeleza ibada ya Hija, alikwenda Uturuki.

Mnamo 1924, alirudi Uchina akiwa amebeba vitabu 600. Baada ya kurudi nyumbani, alianza kufasiri au kutarjumu vitabu mbalimbali, akitumia miaka 40 ya maisha yake katika shughuli hiyo

Pia aliandika kamusi ya Kiarabu hadi Kichina, ambayo ilibaki kuwa marejeleo pekee katika uwanja huo kwa miaka 30.

Kazi yake kuu, ingawa, ilikuwa tafsiri ya Qur'ani Tukufu. Ilikuwa ni tafsiri ya kwanza ya Qur'ani nzima kwa Kichina, ambayo ilimchukua miaka 20 kuikamilisha.

Tafsiri hiyo ilichapishwa Beijing mnamo 1932, kisha huko Yinchuan mnamo 1942 na Shanghai mnamo 1946.

Sheikh Ilyas Wang Jingzhai alijitolea maisha yake kwa ajili ya Uislamu na Waislamu na ndio maana ana nafasi maalum miongoni mwa Waislamu wa China, wanaomchukulia kuwa mmoja wa maimamu wao wakuu.

Habari zinazohusiana
captcha