IQNA

Tafsiri ya Quran Tukufu kwa Lugha ya Kituruki kwa Kuzingatia Hadithi za Ahl-ul-Bayt

17:42 - June 26, 2023
Habari ID: 3477194
Hojat-Al-Islam Morteza Torabi ni mfasiri wa Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kituruki na amejaribu kutumia wafafanuzi wa Kishia wa Quran Tukufu katika kazi yake.

Alizaliwa katika familia ya kidini katika Kijiji cha Yasi Agha, mkoa wa mashariki wa Uturuki wa Agri, mwaka wa 1962. Alihamia mji mtukufu  wa Najaf, Iraq, akiwa na umri wa miaka 9 na akaingia katika Seminari ya Kiislamu ya jiji hilo, alisoma fasihi ya Kiarabu huko.

Miaka mitatu baadaye, alihamia mji mtukufu  wa Qom nchini Iran na kuendelea na masomo yake katika fani za Fiqh, Usul na falsafa ya Kiislamu katika Seminari ya Kiislamu ya Qom.

Kisha akaanza kutafsiri vitabu vya kidini kutoka Kiarabu na Kiajemi hadi Kituruki.

Hojat-Al-Islam Torabi iliitafsiri Quran Tukufu  katika lugha ya Kituruki kuanzia mwaka 2004 hadi 2009. Sifa inayobainisha ya tafsiri yake ni kwamba kutoka miongoni mwa maana tofauti za aya, amechagua maana ambayo imeegemezwa kwenye Hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Ahl-ul-Bayt (AS).

Pia amenufaika na tafsiri za Qur'ani Tukufu  za Shia kama vile wafasiri wa Safi, Shibr na Majma al-Bayan katika tafsiri yake.

Pamoja na tafsiri hii, Hojat-Al-Islam Torabi aliandika kitabu kiitwacho Quran Tukufu  kutoka kwa Ahl-ul-Bayt (AS).  Mtazamo  ambamo alizungumzia masuala kama vile uhusiano kati ya Ahl-ul-Bayt (AS) na Quran Tukufu  akifundisha na kujifunza Qurani Tukufu,  kusoma Qurani, miujiza ya Qurani, ufunuo na mkusanyiko wa  Tafsrir ya aya za Qurani, ufahamu wa Quran na Kitabu Kitukufu kuwa salama kutokana na upotoshaji wowote.

Katika kitabu hiki, amejaribu kukusanya na kuwasilisha kwa njia mpya maoni ya Waislamu wa Shia kuhusu sayansi za Qur'ani  Tukufu kwa kuzingatia Hadith za Ahl-ul-Bayt (AS).

Hojat-Al-Islam Torabi alitafsiri Qurani kwa Kituruki chini ya usimamizi wa Taasisi ya Utamaduni ya Tarjoman-e Vahy tafsiri ya ufunuo, Ilichapishwa na Kawthar Publications yenye makao yake Istanbul Mwaka 2009.

 

3484081

 

captcha