IQNA

Nakala 28,000 Ya Tafsiri Za Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kiswidi zachapishwa Kuwait

11:02 - September 07, 2023
Habari ID: 3477559
KUWAIT CITY (IQNA) - Jumuiya ya kutoa misaada ya Kuwait imechapisha nakala 28,000 za tafsiri ya Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kiswidi (Sweden).

Shirika la Huduma kwa jamii ya Qur'ani Tukufu,  linalojulikana kama Huffaz, limechapisha tafsiri hiyo kama hatua ya kukabiliana na udhalilishaji wa Qur'ani  Tukufu nchini Uswidi.

Abdul Aziz al-Rifa'ei, rais wa jamii, alisema tafsiri hiyo imetolewa kwa ushirikiano na Scandinavia Education Foundation.

Alisema ni tafsiri sahihi zaidi ya Qur’an Tukufu katika lugha ya Kiswidi

Pia inajumuisha tafsiri ya Kitabu Kitukufu kulingana na ufafanuzi maarufu wa Qur’ani, al-Rifa'ei aliongeza.

Pia alibainisha kwamba timu ya wasomi na watafsiri walishirikiana katika kuitafsiri tafsiri hiyo ya Aya za Qur’an Tukufu .

Al-Rifa'ei ameongeza kuwa jumuiya ya kutoa misaada inapanga kuchapisha na kusambaza maelfu ya nakala nyinginezo za tafsiri za Qur'ani Tukufu  katika lugha tofauti.

 

3485058

 

Kishikizo: sweden
captcha