Hussein Aldaodi, mkuu wa shule ya Alsalamskolan iliyo katika mkoa wa Orebro amesema kamera za siri zimeonyesha watu wawili wakiwasha moto kwa lengo la kuitetekteza shule hiyo.
“Watu wawili waliokuwa wamefunika nyuso zao kwa barakoa walivunja madirisha ya shule na kuwasha moto,” amesema Aldaodi.
Amesema moto haukunea na hakuna aliyejiruhiwa katika tukio hilo kwani hapakuwa na mtu yeyeote shuleni wakati huo. Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tuukio.
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na hujuma dhidi ya Waislamu nchini Sweden na maeneo mengine ya Ulaya.