Ee Mwenyezi Mungu! Niwezeshe na Unipe Nguvu za kufunga (mwezi huu wa Ramadhani wote) na kusimama kwa ibada (zinginezo kama sala n.k.) na Uniepushe na matelezo mbali mbali na madhambi katika mwezi huu, Unidumishe na kukutaja kwa uongozi wako Ewe Mwongozaji wa waliopotea.