IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Kazi za sanaa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran

14:45 - March 24, 2024
Habari ID: 3478566
IQNA - Kazi tisini zilizochaguliwa za sanaa zinaonyeshwa katika sehemu ya sanaa ya Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran.

Seyed Mostafa Zaravandian, mkuu wa sehemu hiyo, alipongeza mapokezi mazuri ya banda la sanaa katika maonyesho hayo.

Alisema zaidi ya kazi za sanaa 1,500 ziliwasilishwa kwa sekretarieti ya maonyesho hayo.

Jopo la wataalamu lilichagua 90 kati yazo kuonyeshwa, alisema.

Amesisitiza kuwa lugha ya sanaa ndiyo njia madhubuti zaidi ya kukuza utamaduni na dhana za Qur'ani.

Maonesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalizinduliwa Jumatano Machi 20 katika ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini (RA).

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza ufahamu Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani.

Huonyesha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

3487698

Habari zinazohusiana
captcha