IQNA

Ujumbe wa Qur'ani

Will Smith asema kisa cha Musa katika Qur'ani kilimvutia sana

15:14 - March 19, 2024
Habari ID: 3478542
IQNA - Mchezaji nyota wa Hollywood, Will Smith amesema amavutiwa sana na Qur'ani Tukufu, na kuongeza kuwa kisa cha Nabii Musa (AS) katika Qur'ani kilikuwa na athari ya kusisimua kwake.

Will Smith asema kisa cha Musa katika Qur'ani kilimvutia sanaKatika mahojiano katika kipindi cha “Big Time Podcast”, alisema kwamba alikuwa aliwahi kusoma Qur'ani nzima katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Smith alifichua hali yake ya kina ya  kiroho na tafakuri wakati anapokumbana na changamoto ngumu..

Alidokeza kuwa amekuwa akipitia wakati mgumu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, jambo ambalo lilimfanya kutafuta utu wake wa ndani. Katika kipindi hiki, alisoma vitabu vyote vitakatifu, pamoja na Qur'ani Tukufu. "Kilikuwa kipindi cha maisha yangu nilipotaka kupanua moyo wangu kadiri niwezavyo ili niweze kukumbatia idadi kubwa zaidi ya watu."

Smith alionyesha kupendezwa sana na usahili wa Qur'ani Tukufu na akasimulia jinsi simulizi ya Nabii Musa (AS) ilivyomgusa sana. "Nilishangaa kupitia marejeo mengi kuhusu Nabii Musa (radhi za Allah ziwe juu yake-AS-) katika Qur'an Tukufu," alisema huku akibainisha kuwa hili ni jambo la kuvutia.

Alisema kwamba kisa cha Nabii Musa (AS) kilikuwa na taathira ya kuvutia kwake. “Ninapenda usahili wa Qur'anI kwani rahisi kuifahamu na mambo ndani yake yako wazi kabisa, na hivyo ni rahisi sana kumaliza kusoma. Nilishangaa kwamba kila kitu kilionekana kama hadithi moja... kuanzia Torati hadi Biblia hadi Qur'an,” alisema huku akisisitiza kwamba hakuwa na ufahamu wowote kuhusu nukta hizo.

Smith, mmoja wa nyota maarufu waa Hollywood ambaye  filamu zake zimeingiza zaidi ya dola bilioni 9.3, pia alizungumza juu ya utajiri wake wakati wa mahojiano. Smith alisema kwamba alihisi kuwa nusu ya kwanza ya maisha yake ilikuwa sehemu ya kukusanya mali, na kwamba nusu ya pili ilikuwa ikitumia. "Pesa sio kitu ambacho watu wanahitaji zaidi, na kwa hivyo katika hatua hii ya maisha yangu nataka kutoa ujuzi wangu na uzoefu. "Upendo na urafiki ndio njia pekee ya sisi kuwa hapa kwa furaha."

3487643

captcha