IQNA

Njia ya Ustawi / 5

Muongozo wa Tarbiyah (Malezi)

16:48 - November 21, 2023
Habari ID: 3477924
TEHRAN (IQNA) - Njia moja ya Tarbiyah, yaani kurekebisha au kuboresha tabia ya mtu ambayo imesisitizwa ndani ya Qur'ani Tukufu, ni kumfundisha mtu kivitendo na kiroho kwa namna ambayo mizizi ya maovu ya kimaadili iondolewe katika tabia yake.

Ikiwa mtu atafanya jambo kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu nje au kwa ajili Riya (kujifanya kuwa mtu mwema, mwenye tabia njema au muumini wa kweli mbele ya watu kwa ajili ya kujipatia heshima na kusifiwa) ni kwa sababu ya hofu au ili kupata heshima fulani. Mtu kama huyo anapaswa kusoma Qur'ani Tukufu, pamoja na Aya ya 65 ya Surah Yunus, "Hadhi zote ni za  Mwenyezi Mungu," na Aya ya 165 ya Surah Al-Baqarah, “Na laiti walio dhulumu wakajua watakapo iona adhabu kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu,” kutambua kwamba utukufu na uwezo ni wa Mwenyezi Mungu tu.

Kwa njia hiyo, hakutakuwa na nafasi kwa mtu kuonyesha Riya na kujifanya. Asingemwogopa mtu yeyote wala hangeweka matumaini kwa wengine.

Ikiwa hakika kama hiyo itaingia moyoni mwa mtu, itaondoa maovu yote ya kiadili na kuimarisha wema.

Mungu amesema mara nyingi ndani ya Qur'ani Tukufu kwamba Yeye pekee ndiye mmiliki wa kweli wa kila kitu kilichoko mbinguni na ardhini. Wakati mtu anaelewa dhana hii kwa kweli, angetambua kwamba hakuna kiumbe kisichojitegemea kwa Mungu na kwamba viumbe vyote vina mwisho na vinahitaji na vinamtegemea Mungu. Mtu kama huyo hatatafuta chochote ila ukweli na Mungu.

Aya za Quran zinazofuata njia hiyo ya elimu katika maadili ni nyingi.

Ni pamoja na zifuatazo:

Aya ya 8 ya Surah Taha: “Mwenyezi Mungu! Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Yeye ana majina mazuri kabisa."

Aya ya 7 ya Surah Sajdah: “Yeye ndiye aliyeumba kila kitu kwa namna bora zaidi.”

Aya ya 111 ya Surah Taha: “Nyuso zitanyenyekea mbele ya Mwenyezi Mungu wa Milele na Aliyekuwa Mwenyewe.”

Aya ya 116 ya Surah Al-Baqarah: “Wote wanamtii.”

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu
captcha