IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu /13

Kitabu Kisichokuwa na Shaka

18:49 - July 08, 2023
Habari ID: 3477255
TEHRAN (IQNA) – Mwenyezi Mungu, katika Aya ya 2 ya Surah Al-Baqarah, anaitaja Qur'ani Tukufu kuwa ni kitabu kisicho na shaka ndani yake. Je, kuna uhakika gani juu ya Qur'ani Tukufu ambayo aya hii inaizungumzia?

Aya ya 2 ya Sura Al-Baqarah inasema: “Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa Muttaqin (wachamungu).”

Hii ina maana kwamba aya na dhana za Qur'ani Tukufu  ni za namna ambayo haziachi nafasi ya shaka. Hii inaweza kuchambuliwa kutoka nyanja mbili:

  • Maudhui ya Quran:

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 13 na 14 ya Sura At-Tariq: “Hakika hii (Qur’ani) ni kauli ya kupambanua, Wala si mzaha."

Haya is majigambo bali ni ukweli kwani tunaona kuwa baada ya zaidi ya karne 14 tangu kuteremshwa kwa Qur'ani hakuna aliyeweza kudai kuwa anaweza kuleta hukumu iliyo bora kuliko zile za Qur'ani au kupingana na Kitabu kitukufu.

  • Njia ya kujieleza kwa ufasaha na fasaha katika Quran: Wakati fulani watu huwa na mitazamo mizuri na sahihi akilini lakini hawawezi kuieleza vizuri. Qur'ani Tukufu sio tu ina mafundisho tukufu na ya hali ya juu bali pia inayaeleza kwa ufasaha wa hali ya juu.

Mambo katika aya hii yanasaidia mtu kutambua hadhi tukufu ya Qur'ani Tukufu. Hapa kuna mambo mawili kati ya hayo:

  • Katika Aya hii kiwakilishi cha mbali kinatumika kurejelea Qur'ani Tukufu, ambacho kinaonyesha ukuu wa Kitabu kitukufu. Qur'ani Tukufu iko hapa pamoja nasi na tunaweza kuipata kama kitabu lakini ukweli wa Kitabu Kitakatifu ni wa hali ya juu sana na wa kustaajabisha na ndio maana Mungu anairejelea Qur'ani Tukufu kwa kiwakilishi "hicho".
  • Aya pia inasema Qur'ani Tukufu ni ya Muttaqin (wachamngu). Ukweli ni kwamba Qur'ani imeteremshwa kwa ajili ya mwongozo wa watu wote lakini ni wale tu wanaotafuta haki na wenye mioyo safi na nafsi safi ndio wanaoweza kufaidika nayo ipasavyo. Mvua inaponyesha kwenye bustani husababisha mimea mibichi kukua na hatimaye kuleta mazao na faida nyinginezo, lakini inaponyesha kwenye dampo la takataka, husababisha uvundo tu.
captcha