IQNA

Waislamu Marekani kuswali mbele ya Ikulu ya White House

15:49 - January 24, 2018
Habari ID: 3471369
TEHRAN (IQNA)-Waislamu nchini Marekani wamepanga kuswali mbele ya Ikulu White House mjini Washington DC na kisha kufanya maandamano makubwa ya kulalamikia ubaguzi wanaotendewa na utawala wa Rais Donald Trump.

Kwa mujibu  Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) mjumuiko huo wa Jumamosi 27 Januari utawaleta pamoja mamili ya Waislamu Wamarekani, wahajiri, wakimbizi na wanachama wa jumuia za kiraia. Maandamano hayo yameitishwa kwa munasaba wa mwaka moja amri ya Trump ya kuwapiga marufuku Waislamu kutoka nchi kadhaa kuingia nchini humo.

CAIR inasema marufuku hiyo ya Trump imepelekea Waislamu wabaguliwe na kuzuia watu wengi kujiunga na jamaa zao walio Marekani.

Watuo kutoka nchi za Waislamu ambao wameathiriwa na marufuku hiyo ya Trump wanatazamiwa kuzungumza katika mkusanyiko huo.

Wiki moja bada ya kuingia madarakani Januari 20 mwaka jana, Rais Donald Trump wa Marekani alitia saini amri ya kuwazuia Waislamu wa nchi kadhaa kuingia nchini humo. Baada ya kutoa saini hiyo iliyoonyesha uhasama na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu, Trump alitaja utiwaji saini sheria hiyo kuwa hatua kubwa

Kwa mujibu wa sheria wakimbizi kutoka Syria watazuiwa kuingia Marekani huku wahajiri kutoka nchi za Waislamu kama vile Sudan, Somalia, Iraq, Iran, Libya na Yemen walipigwa marufuku kwa muda kuingia Marekani.

Mwezi Septemba sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho ambapo, Trump sambamba na kutoa amri mpya dhidi ya uhajiri aliwajumuisha raia wa nchi za Korea Kaskazini, Chad na Venezuela katika orodha ya raia wa nchi sita za Waislamu ambazo ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Libya, Somalia, Syria na Yemen kuwa wasiotakiwa kuingia Marekani.

3465033

captcha