IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Msikiti ni kituo cha kuandaa mazingira kwa ajili ya kuleta ustaarabu wa Kiislamu

23:05 - August 21, 2016
Habari ID: 3470535
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, msikiti unapaswa kuwa kituo cha kumjenga mwanadamu kukabiliana na adui, kuujenga moyo kimaanawi na kidunia, kuongeza muono na kuandaa mazingira kwa ajili ya kuleta ustaarabu wa Kiislamu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo Jumapili ya leo kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Msikiti alipokutana na Maimamu wa Swala za Jamaa wa mkoa wa Tehran na kubainisha kwamba, msikiti ni chimbuko la utamaduni wa kimuqawama na kituo cha shughuli za kijamii.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akiendelea kuzungumzia umuhimu wa msikiti amesema kuwa, katika historia ya Uislamu, msikiti ulikuwa ni makao makuu ya mashauriano, ushirikiano na sehemu ya kuchukua maamuzi kuhusiana na masuala muhimu ya kijamiii, kisiasa na kijeshi.

Ayatullah Khamenei amezungumzia pia falsafa ya kuainishwa Siku ya Kimataifa ya Msikiti na kueleza kuwa, siku hii iliainishwa na kupasishwa katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC kwa mashinikizo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na kuchomwa moto msikiti wa al-Aqswa na Wazayuni na lengo lake ni umma wa Kiislamu kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel; hivyo siku hii inapaswa kuzingatiwa kwa mtazamo huo huo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyataja Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwamba, ni zilzala kubwa iliyotikisa nguzo za mfumo wa kibeberu na kusisitiza kwamba, kwa baraka za Uislamu wa Kimapinduzi na Mapinduzi ya Kiislamu malengo makuu ya madola yanayotumia mabavu duniani yaani kulidhibiti eneo la Mashariki ya Kati yaligonga mwamba na kivitendo Marekani imekwama katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, kama isingekuwa imani ya wananchi na kushikamana kwao na Uislamu, Iran nayo kama yalivyo mataifa mengine ingekuwa katika mwavuli wa Marekani na madola mengine; na ni kwa sababu hii ndio maana madola hayo yana uadui na chuki kubwa na isiyo na kikomo na imani ya wananchi.

3524358

captcha