Kwa mujibu wa tovuti ya al-Watan, warsha hiyo iliyofanyika Novemba 15 ilifanyika kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kidini Misri chini ya uenyekiti wa Sheikh Abdul Hakim Abdul Khalif, rais wa Chuo Kikuu cha Tanta.
Warsha hiyo ililenga kueneza sera za Wastani za Kiislamu ili kukabiliana na misimamo mikali ya kidini inayonasibishwa kimakosa na Uislamu jambo ambalo limeuchafulia Uislamu jina na kuleta machafuko na migawanyiko katika jamii mbali mbali duniani.
Warsha hiyo imejadili masuala mbali mbali kuhusu vijana na fikra za kidini.